Siku hizi mitandao ya kijamii ina nguvu
sana, tumeshuhudia wasanii wengi wakithibitisha mahusiano yao ya
kimapenzi kupitia social networks kama Twitter na Instagram, siku hizi hii ndio imekuwa njia rahisi zaidi kufahamu ukweli wa tetesi nyingi za mastaa zinazosambaa kila siku.
Uhusiano wa Future na Ciara ulianza
kuweka headlines kwenye social networks hata kabla ya wao wenyewe
kusema chochote, ule ukaribu wao tu kwenye matukio ya picha mitandaoni
na Instagram ilikuwa ni ushahidi tosha kwa mashabiki wengi kuwa kuna kitu kati ya wawili hao… hali hiyo imejirudia tena sema safari hii kwa Future mwenyewe na Blac Chyna ambaye alishawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Tyga.
Wiki iliyopita Blac Chyna alionekana kwenye behind the scene ya video ya Future ‘Stick Talk’ na kwa mujibu wa mtandao wa TMZ wa Marekani wawili hao walionekana tena pamoja jijini D.C kwenye afterparty ya Future… na inasemekana kuwa wawili wao sasa hivi ni marafiki wa karibu sana, je kuna chochote karibu yao!
Kama kawaida mashabiki walichukuwa time na kuanzisha mada juu yao kwenye Twitter… hizi ni baadhi tu ya tweets nilizofanikiwa kuzinasa kutoka Twitter…
Je ni kweli wawili hao wameanza uhusiano wa kimapenzi chini chini? ama ni marafiki tu!
No comments:
Post a Comment