“Haiuzwi kwa wenye umri chini ya miaka 18, kunywa kistaarabu” ujumbe
huu unapatikana katika matangazo yote ya vilevi, na nadhani hilo
linatambulika kwamba pombe si ya vijana chini ya miaka 18. Unywaji wa
pombe ni kawaida kwa watu wengi lakini unakunywa kistaarabu? Sina mpango
wa kukufundisha kunywa pombe wala kukushawishi uanze kunywa Pombe wote
tunajua madhara yanayoletwa kwa unywaji wa pombe wa kupindukia. Leo
tuongelee upande wa pili wa shilingi, faida za unywaji wa pombe kwa
wastani. Narudi unywaji wa pombe kwa wastani.
Magonjwa ya Moyo.
Utafiti kutoka Harvard University Marekani, umegundua unywaji wa
pombe kwa kiasi cha wastani kinasaidia mzunguko mzuri wa damu,hii
inasaidia kuzia matatizo ya moyo na magonjwa ya kiharusi na kupooza
(stroke)
Urefusha Maisha
Utafiti uliofanywa na Catholic University huko Campobasso,
waligundua kuwa kunywa chupa chini ya 4 au 2 kwa siku kwa mwanamme au
mwanamke, kwa asilimia 18 inaongeza muda wa kuishi kama ililipotiwa
na Reuters. Dr. Giovanni de Gaetano wa Catholic University pia alisema
sio mbaya kama unaweza kunywa pombe kidogo wakati wa kula. Makala
nyingine iliyoandikwa na Mediterranean diet, kuwa mvinyo (wine) ni
kinywaji safii wakati wa chakula cha mchana na cha jioni. Lakini usinywe
tu pombe wakati wote.
Inasaidia kuamsha Hisia za Mapenzi
Kama ilivyo Red Wine inasaidia kupunguza kasi ya magonjwa ya
moyo, Mwaka 2009 jarida lililotambulika kama Sexual Medicine, liliandika
kwa utafiti waliofanya asilimia 25 – 30 wanywaji wa pombe hawapati
matatizo ya kushindwa kushiriki tendo. Mkuu wa utafiti , Kew-Kim Chew
Mtaalamu wa magonjwa ya mlipuko kutoka University of West Australia
alifanya utafiti kwa wanaume 1,770 wa Australia, Chew aliwashauri pia
wanaume hao wasitumie pombe kupitiliza sababu bado wanafanya utafiti juu
ya swala hilo kwa kina zaidi.
Pombe huamsha Akili
Utafiti uliohusisha watu zaidi ya 365,000 toka mwaka 1997 iliripotiwa
na jarida la Neuropsychiatric Disease and Treatment watu wanaokunywa
kwa wastani wanauwezo wa kuzuia ugonjwa wa Alzheimer na magonjwa mengine
ya akili. Kiwango kidogo cha pombe kinafanya seli za ubongo ziwe hai
(fit/active) alisema Edward J. Neafsey, Ph.D mwandishi wa Science Daily.
alisema pia hawashauri watu wasiokunywa pombe waanza kunywa pombe. Na
akasema kama wale wanaokunywa wanakunywa kwa wastani basi itawasaidia.
Husaidia Tatizo La Mawe kwenye Kibofu
Kwa wanywaji wa wastani kuna uwezekano wa kupunguza uwezekano wa
kupata tatizo la mawe kwenye kibofu huo ni utafiti uliofanywa na
University of East Anglia, watafiti walisema faida zinaonekana kwa wale
wanywaji wa kawaida na sio waywaji wa pombe kupinduki sababu unywaji wa
pombe kupitiliza huleta matatizo ya kiafya.
Ugonjwa wa Sukari
Tafiti zilizofanywa uholanzi, watu wenye afya wanao kunywa glass
moja au mbili kwa siku wanapunguza uwezekano wa kupata aina ya pili ya
kisukari ukiachilia mbali wale wasiokunywa hata kidogo, wale wanaokunywa
kidogo wana afya zaidi, walisema watafiti hao kupitia Reuters.
Angalizo kujua faida hizi za pombe haina maana kama hujaanza kunywa
pombe uanze sasa na kama wewe unatumia kilevi basi kunywa kwa kiwango
kidogo sababu ni faida kwa afya yako kuliko unywaji wa kupindukia.
Kunywa kistaarabu.
World Of Pl@tnumz
Lifestyle
Wewe ni mtumiaji wa vilevi? haya ni mambo ya muhimu unayopaswa kufahamu kuhusiana na Vilevi.
ABC
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment