Taarifa iliyoripotiwa muda mfupi uliopita na kuthibitishwa na Serikali inahusu Msiba wa Waziri huyo, Abdallah Omar Kigoda ambaye alikuwa Waziri wa Viwanda na Biashara na pia alikuwa Mbunge wa Jimbo la Handeni Tanga kupitia Chama cha Mapinduzi CCM.
Hiyo ni taarifa kutoka Ofisi ya Bunge ikionesha Waziri huyo amefariki leo Jioni katika Hospitali ya Appolo ambako alikuwa akitibiwa.. Serikali iko kwenye Mipango ya taratibu za kusafirisha Mwili wa Marehemu pamoja na Mazishi kwa kushirikiana na Familia ya Marehemu.
RIP Dk. Kigoda… Hapa alikuwa na Mgombea Urais wa TZ kupitia CCM, Dk. John Magufuli.
No comments:
Post a Comment