Ukiacha Mafua,Umeshawahi kufikiria, mchango wa tendo la ndoa katika
afya yako, kabla sijakuambia umuhimu wake, usidhani kuwa tendo la ndoa
linatibu Malaria, muone daktari pale unapojisikia mgonjwa, yapo mambo
kadhaa husaidia afya yako kwa kila tendo moja la ndoa. Hizi ni sababu 7
muhimu unapata baada ya tendo la ndoa.
- Hupungua wingi wa Kalori
Wakati wa tendo la ndoa moyo unaweza kusukuma damu kwa kiasi kikubwa
kuliko kawaida hii husaidia kupunguza kalori ama mafuta katika moyo, kwa
dakika 30 mwili unauwezo wa kupunguza kalori 85 hadi 200,kama unafanya
tendo la ndoa nusu saa kila siku una uwezo wa kupunguza kilo 4.5 kwa
mwaka.
- Ukakamavu wa Mifupa na Misuli
Tendo husaidia uzalishwaji wa homoni ya testeroni ambayo inasaidia
misuli na mifupa pia husaidia nguvu ya mwili, na kukupa hamu ya tendo,
kupungua kwa homini ya testeroni husababisha uchovu, kutokuwa hamu na
tendo la ndoa na msongo wa mawazo.
- Hupunguza uwezekano wa kupata Kansa Ya kibofu
wanaume wanaoweza kupungua manii mwilini mwao mara kwa mara wana
uwezo wa kupunguza uwezekano wa kupata kansa kwa asilimia 30. Kutoa
manii kwa mwanaume inaweza ikawa kwa tendo la ndoa ama kwa kujichua japo
haishauriwi kujichua.
- Muhimu kwa Moyo
Utafiti kutoka Chuo cha Queen Marekani, unaonyesha wanaume
wanaoshiriki tendo mara 3 kwa wiki wanapunguza uwezekano wa kupata
ugonjwa wa moyo na kiarusi kwa asilimia 50. Pia husaidia kupunguza
uwezekano wa kupata shinikizo la damu.
- Hupunguza Msongo wa mawazo (Stress)
Tafiti mbalimbali zimeonyesha,kuna watu wengi baada ya tendo huwa wamepunguza msongo wa mawazo, kwa kiasi kibubwa.
- Kusaidia kinga ya Mwili.
Kuna usemi, mafua ni ugonjwa wa mapenzi , hii ni kwa sababu Kinga
yako ya mwili huongezeka kwa kushiriki tendo mara kwa mara, hii ni kwa
sababu mzunguko wako wa damu kufanya kazi vizuri,kupumua vizuri na
sababu ni moja kati ya zoezi ni rahisi kukusaidia kufungua pua kama
ulipata mafua na kukufanya uweze kupumua vizuri .
- Usingizi wako Muhimu
Unapata tatizo la kukosa usingizi? Inaweza sababishwa na msongo wa
mawazo na mambo mengine mengi. Umewahi kujiuliza kwanini watu wanalala
baada ya tendo, hii ni kwa sababu mwili kwa ujumla unapata kupumzika
(relaxed) baada ya tendo, kemikali inayoitwa serotonini huongezeka
mwilini na kumfanya mtu awe na furaha.
Kwakua hukuyajua haya na Wakati unawaza kukutana na mwenza wako, ni
vizuri kuzingatia afya zenu, kwa kuhakikisha wote ni salama, ninapo
ongelea usalama wa afya wengi wetu wanawaza maambukizi ya ukimwi
pekeake, kuna magonjwa ya zinaa ambayo ni hatari zaidi basi ni vuzuri
kabla hamjarukiana mkapima au mtumie kinga.
No comments:
Post a Comment