Idadi ya raia wa Tanzania
waliofariki katika mkanyagano wakiwa katika ibada ya Hajj nchini Saudi
Arabia mwezi uliopita imeongezeka na kufikia 22,kulingana na waziri wa
maswala ya kigeni.
Mwandishi wa BBC Leonard Mubali anasema kuwa mahujaji wengine 38 kutoka Tanzania hawajulikani waliko.Serikali ya Saudia imesema kuwa takriban watu 769 walifariki katika mkanyagano ,ijapokuwa maafisa kutoka mataifa wanayotoka mahujaji waliofariki wanasema kuwa idadi hiyo ni watu 1,480.
No comments:
Post a Comment