Mwanamitindo na muimbaji, Jokate mwengeleo aka Kidoti ametaka wasanii
kutotumia vibaya umaarufu wao ili wapate ushirikiano katika kazi zao.
Akiongea na kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, Jokate amesema kinachowaponza wasanii wengi ni umaarufu
“Unajua ukiwa maarufu kila mtu akawa anaimba nyimbo yako,
ni rahisi kuvimba kichwa ukajiona wewe ndio wewe, unasahau kabla ya
wewe kulikuwa kuna watu ambao walihit vilevile. Hii ni cycle kwamba leo
umehit, yule kesho,” alisema Jokate
“Wanatakiwa kujua sio kwamba wao watakaa juu milele, hiyo
haipo. Kwahiyo hivyo vitu visikuingie kichwani, cha muhimu ni kufanya
kazi kwa heshima hasa hasa kwa wale watu ambao wapo kwenye industry,” alisisitiza Jokate.
World Of Pl@tnumz
Entertainment
Music Stories
Jokate asema kinachowaponza wasanii wengi ni kuvimba kichwa wanapopata umaarufu.
ABC
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment