Baada ya Rais wa Marekani, Barack Obama kumpatia Kanye West dondoo za namna ya kuwa Rais, wawili hao mida hii walikuwa jijini San Francisco kwa ajili ya kushiriki kikamilifu kwenye ‘Democratic National Convention Fundraiser’… baada ya shughuli nzima kuisha Kanye akaona haitakuwa poa sana kumuacha Rais aondoke mikono mitupu!
Kutokana na tweet ya Kim Kadarshian , inaonekana Rais Barack Obama amejipatia vitatu vya bure kabisa vya ‘Yeezy Boost 350’ kutoka kwenye collection mpya ya Kanye West iliozinduliwa siku chache zilizopita jijini New York!
Tweet iliyowekwa na Kim Kadarshian inaonyesha mabox mawili ya boots za Adidas yakiwa na signature ya Kanye West kwenye kila box na vinoti vilivyoandikwa “Obama” kwenye kila box…Tweet ya Kim Kadarshian ilikuwa inasema;“Special delivery #yeezys”…
Kwa muonekano wa mambo inaonekana Rais Obama sasa hivi atakuwa na pair za kipekee kabisa kwenye kabati lake la viatu, au pengine hii ni namna ya Kanye West kuonyesha shukrani kwa Rais Obama kwa ushauri aliompatia!
No comments:
Post a Comment