Maisha Yake Kwa Ujumla:
Ada Lovelace (Great Mathematician and computer programmer) alizaliwa na 10 desemba 1815 na alijulikana kama Augusta Ada Byron. Ada Lovelace ni mtoto halali na pekee wa Anne Isabella Milbanke na Mshairi(Poet) George Gordon Byron. Mama Ada, Anne Isabella Milbanke alikuwa mtaalamu wa Mathematics na Mumewe Byron alipendelea kumuita mkewe "Princess Of Parrallelograms", Byron alisisitiza kuwa mwanae Ada alikuwa anapenda sana hisabati na alikuwa anafundishwa na mama yake kwa siri utafiti wa hisabati ambao kwa wakati huo ilikuwa ni vigumu kumpata mtoto wa kike akijifunza kuhusu hisabati.
Maisha ya ndoa ya wazazi wake:
Anne Isabella Milbanke aliolewa na Byron, Isabella hakuwa na furaha katika maisha ya ndoa. Isabella alitengana na mumewe baada ya wiki kadhaa kuzaliwa mtoto wao ada, Miezi michache baadae bwana Byron aliondoka na kuelekea uingereza. Baadae alielekea ugiriki na alifariki huko, mwanae Ada akiwa na miaka 8. Ada hakuwahi kumuona baba ake kwani walitengana na mama yake wakati akiwa hana utambuzi.
Malezi yake:
Ada alilelewa na kwa maadili mema katika miaka ya 1800, mama yake alimuendeleza kipaji chake kwa kumfundisha na kumtafutia walimu kumsaidia kuelewa zaidi sayansi na hisabati. Wakati huo kulikuwa na changamoto kubwa, kwani ilikuwa sio rahisi kwa mwanamke au mdada kuonekana akisoma masomo hayo. Katika kukua kwake Ada alionyesha kipaji kikubwa cha hisabati na lugha, alipata maelezo ya msaada kutoka kwa William Frend(Social Informer), William King(Family Doctor), pamoja na Mry Somerville(Scotish Astronomer)
Maisha yake pamoja na ugunduzi wake:
Akiwa na umri wa miaka 17, Ada alikutana na Charles Babbage, (A Great Mathematician and Invetor) na walikuwa marafiki. Babbage alikuwa mshauri wa ada kwa kipindi hicho. Kupitia Babbage, Ada alianza kusoma Advanced Mathematics katika chuo cha kikuu "London University" kilichomilikiwa na Augustus De Morgans.
Ada alivutiwa na mawazo ya Babbage aliyojulikana kama "Baba wa Computer" ambae alikuwa mgunduzi wa injini tofauti tofauti ambazo zilisaidia kurahisisha hesabu za hisabati. Ada alipata nafasi ya kuangalia mashine ambayo ilibuniwa na Babbage kabla ya kukamilika, alivutiwa nayo ambapo baadae pia Babbage aliunda kifaa kingine kilichojulikana ka "Injini Ya Uchambuzi" - (Analytical Engine) ambayo ilishughulika na hesabu tata zaidi.
Ada alitafsiri makala ya Babbage ya Analytical Engine ambayo iliandikwa na muitaliano Luigi Federico Menabrea kwenye Jarida la Uswisi, na kuongeza vitu ama ugunduzi wake mwenyewe kwenye machine hiyo. Makala yake ilichapishwa kwa mara ya kwanza kwa lugha ya kiingereza mwaka 1843 katika jarida la English Science Journal na alitumia vifupisho vya majina yake katika chapisho hilo kama A.A.L - Augusta Ada Lovelace.
Makala zake pamoja na machapisho:
Katika chapisho lake Ada alielezea jinsi gani Codes zinaweza kuundwa kwa ajili kifaa ili kushughulikia Herufi na pamoja namba. Pia alielezea dhana mbinu kwa ajili ya injini programu za komputa zinazotumika leo. Kwa ajili ya kazi yake,Ada alichukuliwa na anaendelea kuchukuliwa kama Mgunduzi wa kwanza wa Programu za komputa.
Makala ya Ada alivuta sana hisia za watu wakati akiwa hai, katika amaisha yake, Ada alijaribu kuendeleza miradi mbalimbali ikiwa pamoja na miradi ya hisabati ambayo mpak leo inaendelea katumika katika michezo ya bahati nasibu(Kamari)
Kifo Chake:
Ada alifariki kutokana na Kansa ya kizazi(Uterine Cancer) akiwa london Novemba 27, 1852 na alizikwa pembeni ya baba yake katika makaburi yaliyoko kanisa la Mtakatifu Maria Magdalena yaliyoko Nottingham, Uingereza.
Makala hii imeandaliwa na:
Walter V. Faustine.
October, 18 2015 - Sunday
No comments:
Post a Comment