Mvulana wa umri wa miaka 14 nchini
Marekani, aliyegonga vichwa vya habari baada ya kukamatwa kwa kupeleka
saa ya kujitengenezea shuleni, amekutana na Rais wa Sudan Omar
al-Bashir.
Ahmed Mohamed na familia yake walilakiwa katika ikulu
ya rais katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum Jumatano, kwa mujibu wa kituo
cha redio cha serikali.Mvulana huyo alifurushwa darasani na kutiwa pingu baada ya mwalimu wake kudhani saa hiyo ilikuwa bomu.
Kukamatwa kwake kulishutumiwa sana. Polisi hawakumfungulia mashtaka yoyote.
Babake mvulana huyo, Mohamed Hassan al-Sufi, ni mhamiaji kutoka Sudan anayeishi Marekani.
No comments:
Post a Comment