Breaking News
recent

Q-chief kuwashirikisha Diamond na TID kwenye wimbo wake mpya.

Q-chief amemshirikisha TID kwenye wimbo wake mpya ambao bado wapo kwenye mazungumzo na mkali wa ‘Nana’ Diamond ili aikamilishe colabo ya wimbo huo.
Akiongea na mtandao wa Bongo5 Q-chief amesema baada ya kumaliza tofauti zake na member mwenza wa kundi lao la zamani la ‘Top Band’ TID ameamua kumshirikisha kwenye wimbo wake mpya ambao tayari TID amesharekodi
“Lakini tumemaliza tofauti zetu, sisi kama watu wazima tunajitambua na nikamwambia hebu tujaribu kufanya ngoma fulani kama aina ya mdumange, ili tujaribu kurudi nyumbani kwa watu wetu. Na ukiangalia wasanii wa kwanza waliofanya vizuri ni Q Chillah na TID.”  Alisema Q
Pia aliongeza kuwa tayari wamemtumia wimbo huo Diamond ili aone anaingiaje
“Kwahiyo tumefanya project kwa Abby Daddy, na Abby Daddy naye yupo kwenye mazungumzo na Diamond ilikuwa aingie kwenye hii ngoma. Tayari TID amemtumia ngoma kwa sababu ametoka kuchukua zile tuzo inabidi tumpongeze halafu tumpe kama wiki moja na nusu then tujue kama ataingia au vipi. Kwa sababu tunajua anaweza kuwa busy sana lakini ile ngoma tayari ni hit. Kwahiyo mwezi wa kumi na moja watu watapata vitu vizuri.” Alisisitiza Q-chief.
ABC

ABC

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.