Breaking News
recent

Said Fella kuibua vipaji vipya kwenye Kata yake ya Kilungule, Kuachia video ya kundi jipya baada ya uchaguzi.

Mgombea wa udiwani kata ya Kilungule jijini Dar es Salaam, Said Fella ameelezea mpango wake wa kuinua zaidi vipaji vya vijana  ambapo tayari ameunda kundi jipya la wasanii ambao wataachia video mpya baada ya uchaguzi.
Akiongea na Enewz, Fella amesema kundi hilo linaitwa ‘Salam TMK’ litafanya kazi kama ambavyo walikua wanafanya zamani na TMK wanaume Family

“Pale mkubwa na wanawe kuna vijana 8 vijana hao tunawaita salam Tmk, hao wameimba wimbo mmoja itakua kama zamani tulivyokua tunafanya TMK wanaume Family, kwahiyo ni kundi lakini litaitwa Salam Tmk, kwahiyo ngoma yao mpya nadahani itatoka baada ya vile vile uchaguzi kwasababu video tumeshafanya Zanzibar na tumerudi producer kafanya shirko, kuiandika nimeiandika mwenyewe” Amesema kiongozi wa Mkubwa na Wanawe.

Katika hatua nyingine Fella ameelezea mpango wa kuinua vipaji vya vijana wa Kata ambayo anawania udiwani, Kata ya Kilungule ambapo amesema tayari amepata viajana karibia 50 wenye vipaji tofauti ikiwemo wasanii wa Tradition, wengine Bongo Fleva, Taarabu, HipHop na wacheza mpira Japo hawa hawatounganishwa na wasanii ambao anawasimamia chini ya Mkubwa na wanawe.
ABC

ABC

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.