Je ni kweli mnataka kuwa marafiki?
Jaribu kujiuliza kama kuna ulazima wa wewe na yeye kuwa marafiki, na mtaweza kuvumilia mipaka ya urafiki, kumbuka hamuwezi kuwa marafiki kama marafiki wengine, tayari mmepitia mahusiano mnafahamiana zaidi ya urafiki, kuwa makini kabla hujaamua kuanza urafiki huo mpya.
Una uhakika na hisia zako?
Upo wakati unaachana na mtu sababu tu, kuna mambo mengi yalisababisha mahusiano hayo kuisha, je bado unahisia za mapenzi na mtu huyo, na unadhani utaweza vumilia nyie kuwa marafiki tu, kama huwezi na unahitaji kuendelea na maisha yako ni vizuri ukapingana na swala la nyie kuwa marafiki sababu urafiki huo hautadumu.
Jichanganye nae katika Vikundi.
Mkiwa katika kundi la marafiki, ni salama zaidi hasa kama mna marafiki wa aina moja, marafiki zako na marafiki zake pamoja, kutoka chuoni au Darasa moja ,
Bado una Wivu nae?
Kama bado unajisikia vibaya ukimuona na mtu mwingine na ni wazi bado unampenda, na ni vizuri kama utakaa nae mbali,na kama yeye anaona wivu ukiwa na mtu mwingine basi si sawa mkiendelea kuwa marafiki sababu bado mnahitaji kuwa zaidi ya marafiki.
Bado Mnakumbuka mlipotoka?
Mnapokumbuka mambo mliyofanya pamoja, kama mitoko ya pamoja kwenye sherehe mbalimbali,matamasha mlienda pamoja na vitu vingine vyote ambavyo vinabeba kumbukumbu yenu si vizuri kuviongelea kama mmeamua kuwa marafiki, si vizuri kuongelea mliyoamua kuyaacha, mnaweza mkarudi nyuma mlipotoka.
Vitu muhimu vya kuzingatia ni, kujiuliza kama mlishindwa kuwa wapenzi kwanini muwe marafiki sasa na kwanini? Kitu cha muhimu ni kuendelea na maisha sababu maisha hubadilika na watu hubadilika pia
No comments:
Post a Comment