Selfie sio msemo mpya kwa watu wengi, upigaji huu wa picha umekuwa
maarufu kwa watu wengi hasa kwenye mitandao ya kijamii duniani kote,
hakuna kanuni za kupiga selfie wala sheria ila kuna mambo machache ya
kuzingatia ukichukua selfie.
- Selfie sio Photoshop: usiwaze kuhusu ubora wa
muonekano wako, uwe na muonekana wa asili (natural), selfie ukiwa umetoka
kuamka au ukiwa na kikombe cha chai mezani si lazima kujipamba ili
uonekane mrembo/mtanashati zaidi
- Mwanga: picha nzuri ni mwanga mzuri, selfie nzuri
ni zile zinazopigwa nje zaidi kuliko ndani, mwanga mwingi sana au mdogo
sana unaweza fanya picha iwe ina mwanga sana au iwe na giza sana mda
mzuri wa selfie ni asubuhi na jioni kabla jua halijazama.
- Usikunje midomo yako: maarufu kama “duck face” watu
wengi hasa wadada wanapenda sana staili ya kukunja midomo yao, sura
yako haitoonekana kiasili (natural)
- Selfie Bafuni: vioo vya mabafu ndio sehemu za
selfie kwa baadhi ya watu, kupiga picha kwenye vioo vya bafuni katika
hotel au migahawa mikubwa si poa, selfie bomba haipigwi maliwatoni.
- Usidanganye kulala kwenye selfie: Hii watu hupiga
waonekane kama kuna mtu mwingine kapiga hiyo picha kitu ambacho si
kweli, haumdanganyi mtu linapokuja swala la selfie , mikono yako, pozi
lako ni ishara tosha kwamba umejipiga picha mwenyewe.
- Kuwa wa tofauti: badilisha sehemu unazopiga picha
kila siku, chumbani, ofisini, barabarani zinaweza kuwa ni sehemu za kila
siku, selfie chini ya maji ukiwa ufukweni juu ya majengo marefu, ila
uwe makini na usalama wako.
- Background: kuwa makini na sehemu uliyochagua na
nini kitaonekana nyuma yako, mfano nguo nyuma ya mlango, wako au chumba
kisicho na mpangilio mzuri picha moja anaweza ikakuvunjia heshima ama
kuwapa nafasi ya watu kukuelewa vibaya.
No comments:
Post a Comment