Nilipokutana na somo hili CNN, sikutaka kuliacha linipite nikaona si
vyema nikanyamaza na kuamua kuliandika hapa, Hakuna kitu kigeni kwenye
swala la kubusu kwa lugha iliyozoeleka Kiss,ila sio kiss la mkono au
juu ya paji la uso, naongelea kiss ambalo ni Deep, wanaita French kiss
hii watu hufanya kama mazoea tu kwa wapenzi, kuna mambo unatakiwa kujua
kuhusu kubusu zaidi ya kubadilishana mate na mwenza wako.
Kubusu kunahamsha Homoni ya Furaha
Mwanasayansi Demirjian, alielezea unapokuwa na huzuni au kuwa na
msongo wa mawazo moja kati ya vitu huleta furaha ukiacha kukutana
kimwili na mwenza wako basi kubusu,kubusu kunaleta furaha inakufanya
ujisikie vizuri,wakati wa kubusu kuna aina ya kemikali zinajitengeneza
mwilini serotonin,Depamine na oxytocin ambazo humfanya mtu ajisikie
vizuri kama vile mtu anavyojisikia akiwa ametoka kufanya mazoezi.
Husaidia Maumivu ya kichwa
Kubusu kunamfanya mtu awe ame relax hii inafanya mzunguko wako wa
damu kwenda taratibu, na kuufanya mwili ujitibu taratibu kwahiyo ukiacha
maumivu yale makali ambayo yanahitaji daktari, ukiwa na maumivu ya
kawaida ya kichwa usiogope kupata busu unaweza kupona maumivu.
Ubovu wa Meno au Kutoboka kwa Meno
Kubusu huchangia kubadilishana kwa mate na maji maji yote ya
mdomoni, na unapokiss mate mengi yanajitengeneza mdomoni, na mate mengi
husaidia kuondoa wadudu wanao ozesha meno, alisema hayo Demirjian, ila
ni lazima kila mtu na mwenza wake wawe makini na midomo yao kwani harufu
mbaya haitowafanya wafurahie kubusu. Wanawake wengi hupenda wanaume
wasafi na wenye meno masafi na kuna baadhi ya wanawake huangalia hata
mpangilio wa meno ya wanaume hao.
Mazoezi kwa Misuli ya uso
Misuli yako ya kichwa na taya hutumika wakati wa kubusu hii kusaidia
kufanya misuli yako ya uso ivutike na kukaza kwahiyo inasaidia kutopata
makunyanzi mapema usoni, ni moja kati ya zoezi kwa uso.
Kusaidia kufurahia Tendo la ndoa
Kwa watu wanaopenda kubusu wanaelewa hili, ukikutana na mtu kwa mara
ya kwanza na hajui kukiss basi hawezi kuwa mzuri kitandani,ila busu zuri
linafanya watu wawili wafurahie tendo sababu ngozi ya midomo inahamsha
hisia kirahisi zaidi. na inasemekana wanaopenda sana kubusu ni watu
wanaopenda pia kufanya mapenzi kuliko watu wengine. Na yapo mahusiano
ambayo yalishawahi kuvunjika sababu tu mwenza mmoja alikuwa hajui
kubusu vizuri.
Busu husaidia shinikizo la damu.(blood Pressure)
Kubusu kunahamsha hisia kali mwilini na hii kusaidia moyo wako
kusukuma damu kwa hali ya kawaida na kiafya hii hupunguza shinikizo la
damu na moyo wako unafanya kazi inavyotakiwa alisema haya Demirjian.
ABC
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment