Breaking News
recent

Khole Kardashian akanusha kurudiana na Lamar Odom.

Mbali ya kufuta kesi ya kuomba talaka yake kwa Lamar Odom, Khole Kardashian ameibuka na kusema kuwa yeye na Lamar hawajarudiana.
Akiongea na jarida la People, Khole amesema ameamua kumsupport Lamar tangu amepata matatizo [Nov.13] lakini hawajapanga kurudiana
“Nataka watu waelewe kuwa swala la mimi na Lamar kurudiana halipo kabisa kwenye mawazo yetu, wala hatujifikiri kama wapenzi au tuna mahusiano kwa sasa”  Alisema Khole.
Kuhusu kufuta kesi ya Talaka, Khole amesema amefuta kwakuwa hana haraka na talaka na hana mpango wa kuolewa hivi karibuni.
ABC

ABC

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.