Ndoa ya mcheza kikapu wa NBA Lamar Odom na Khloé Kardashian iliyokua
kwenye mawe imepona kufuatia kuugua kwa mcheza kikapu huyo, imeripotiwa
kuwa wanandoa hao wameifuta kesi ya talaka ya ndoa yao.
Siku moja baada ya Khloé kumpiga chini aliyekuwa mpenzi wake wa sasa
James Harden ili kupata muda wa kumuuguza Lamar Odom wawili hao
waliofunga ndoa mwaka 2009 japo ilivunjika baada ya miaka minne wameamua
kuendelea kuwa mume na mke.
Kwa mujibu wa TMZ, mwanasheria wa Khloé aitwaye Laura Wasser , Siku
ya Jumatano (Oct. 20) alienda kwa hakimu kuomba kusitisha kesi hiyo huku
wote wakiwa wamesaini hati ya kukubali kufuta kesi ya kuvunja ndoa yao,
na jaji alifanya kama walivyoomba.
Khloé alifungua kesi hiyo ya kudai talaka mwezi December mwaka 2013.
World Of Pl@tnumz
Entertainment
Music Stories
Khloé Kardashian na Lamar Odom waifuta kesi ya Talaka, kuendelea kuwa Mume na Mke.
ABC
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment