Preshow kabla ya sherehe zenyewe za utoaji wa Tuzo za MOBO ‘Music of
Black Origin’ imefanyika usiku wa jana huko London ambapo washindi wa
tatu wa kwanza wa tuzo hizo walitangazwa.
Mwanamziki wa UK, Shakka alishinda tuzo ya ‘Best RnB/Soul Act
award’, Binker na Moses walishinda tuzo ya ‘Best Jazz Act’ na Muimbaji
wa ‘Airborne’ Faith child aliibuka mshindi wa Tuzo ya ‘Best Gospel Act’Sherehe yenyewe ya utoaji wa Tuzo hizo itafanyika jumatano ya wiki ijayo [Nov. 4] ambapo kutoka Afrika wasanii wanaowania kipengele cha Best African Act ni pamoja na Shatta wale, Davido, AKA, Wizkid na Fuse ODG.
No comments:
Post a Comment