Mshindi wa Tuzo ya Afrimma ‘Best Female East Africa’ Vanessa Mdee
amesema msanii kushinda Tuzo nyingi haimaanishi kuwa anafanya vizuri
sana.
Vee Money ameyasema hayo wakati anafanya mahojiano na kipindi cha
Planet Bongo cha East Africa Radio ambapo alimtolea mfano Wizkid,
Alisema
“Msanii kuwa na Tuzo, kwa mfano tumuangalia WizKid ana tuzo
chache, lakini muziki wake unafanya vizuri dunia nzima, Drake
anamtafuta, Swizbeat anamtafuta, Alicia Keys ana mtafuta na ratiba yake
iko busy mwaka mzima, So haijalishi”
Katika hatua nyingine Vee alielezea experience aliyoipata kufanya kazi na 2face Idibia kwenye Coke Studio “Tulivyokuwa
tunashoot nilikuwa na 2face, wengine walikuwa hawajafika, sijawahi
kufanya kazi na msanii mkubwa kama yeye, ana heshimu kazi, nimejifunza
kitu toka kwake mkarimu, na kuna nafasi kubwa kwa wasanii wa Afrika
kufika mbali" alisema mwimbaji huyo wa Never Ever.
World Of Pl@tnumz
Entertainment
Music Stories
Vanessa Mdee amesema msanii kushinda Tuzo nyingi haimaanishi kuwa anafanya vizuri sana
ABC
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment