Breaking News
recent

Utafiti unaonesha Wanawake wenye makalio makubwa wapo vizuri kichwani na kiafya.

Uuuuuh, nashusha pumzi kabla sijaanza na hii, moja kati ya kitu sikuwahi kufikiri wala kuwaza kuna uhusiano gani na migongo mikubwa nadhani nikisema migongo mikubwa unanielewa, na akili ya mtoto wa kike na afya yake. Inachanganya kidogo lakini kutoka chuo mahili dunia nzima chuo cha Oxford  Marekani kilifanya utafiti juu ya swala hili. Haya yaliandikwa kwenye allwomentalk.com
Taarifa zilizotolewa na ABC News zinasema wanawake waliojaliwa  makalio makubwa  wana kiwango kidogo cha  cholesterol na wana uwezo mkubwa wa kuyeyusha sukari mwilini mwao kwahiyo ni mara chache wanawake wa aina hii wanapata ugonjwa wa moyo au sukari. Kuwa na makalio makubwa unahusishwa na wingi wa aina ya mafuta kitaalamu wanaita “Omega 3 fats” na kazi yake ni kusaidia ufanyaji kazi wa ubongo.
Utafiti huo uliofanywa kwa wanawake wapatao 16,000 inasemekana watoto wanaozaliwa na wamama waliojaliwa makalio makubwa na maumbile makubwa wako vizuri kiakili kuliko wamama walio na maumbile ya kawaida (less curvy)
“Professor Konstantinos Manolopoulos, wa Oxford University ambaye ndie aliyeongoza utafiti huo alisema  wanawake walio na makalio makubwa wanakiwango kikubwa cha “leptin” aina ya protein inayosaidia kumpatia mtu nguvu kutoka kwenye mafuta yaliyojikusanya mwilini na husaidia uchochezi wa homoni aina ya “dinopectina” na sifa za kupambana na ugonjwa wa kisukari .
Watafiti walielezea kuwa uchunguzi huo ulifanywa pia katika vyuo vikuu miji ya California na Pittsburgh  na waligundua pia wanawake wenye viuno vidogo, makalio makubwa na hips kubwa  hapa naongelea wale namba 8, kama ilivyozoeleka kwa wengi,hawa wana uwezo wakuishi maisha marefu pia. Na walisema utafiti huu hausishi watu wenye makalio ya bandia.
ABC

ABC

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.