Mkali wa Movie kwenye Kiwanda cha Bongo Movie Tanzania, Mohamed Mwikongi ambaye wengi tunamfahamu kwa jina la Frank ni moja kati ya watu maarufu waliojitokeza kugombea Ubunge katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika October 2015.
Frank ambaye ni mgombea Ubunge wa jimbo la Segerea kwa tiketi ya chama cha ACT Wazalendo October 12 2015 ameingia katika headlines baada ya kuonekana akitumia usafiri wa Daladala.
Ikafanyika na exclusive interview na Frank ambapo alijibu pia sababu ya yeye kuonekana kwenye Daladala akifanya Kampeni zake…Unadhani huo ni usafiri wake wa kila siku au ndio mambo ya Kampeni? >>> “Huu ni utaratibu ambao ninao, hii ni daladala kwa daladala… ni fursa ya kukutana na watu wengi zaidi na kufahamu changamoto zao ambazo zinawakabili katika usafiri huu ikiwemo foleni, mimi daladala sijaanza kupanda wakati huu wa Uchaguzi, hata kabla ya Uchaguzi huwa naacha gari yangu nyumbani na kupanda daladala ili kupata idea za filamu”>>> Frank.
No comments:
Post a Comment