Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho, amejitetea kuwa kinachodhaniwa ni lugha
mbovu aliyotumia baada ya kushindwa na Southampton ni kwa kuwa
Kiingereza si lugha yake ya mama.
Mourinho alifungiwa mechi moja na kupigwa faini ya Pauni za Uingereza
50,000 na shirikisho la Kandanda la Uingereza. Alidai kuwa maafisa wa
kandanda nchini humo wanaogopa kuipa timu yake penalti inayostahili.
Madai ya Morinho yalitolewa baada ya tume huru maalumu kutoa sababu za
adhabu hiyo kutolewa na FA. Kocha huyo machachari wa Chelsea
hakuhudhuria kilichomwadhibu lakini alituma taarifa ya maandishi
kujitetea. Alikiri kuwa alikosa adabu lakini akakanusha kuwa alitilia
shaka hadhi ya refa Robert Madley. Huku akijitetea, Mourinho alisema
kuwa makosa yaliyompata ni sawa na yale yaliyowahusu makocha wengine
watano wa Premier League. Mbali na kukosoa kiwango cha faini aliyotozwa,
Mourinho pia alisema kuwa kupigwa marufuku uwanjani kwa mechi moja,
ambako kumeahirishwa kutekelezwa kwa mwaka mmoja, “kulimshangaza”.
Wenger hakuchukuliwa hatua yoyote alipomsukuma Mourinho katika eneo la
wakufunzi katika Stamford Bridge Oktoba mwaka 2014.
No comments:
Post a Comment