Aubrey Graham “Drake” alizaliwa Oktoba 24 kwa jina la kisanii, msanii aliefikia mauzo ya platinamu kwa mwaka 2015, ukiyatazama maisha ya Drake tangia utoto wake na maisha aliyopitia kabla hajawa msanii mkubwa ukitazama maisha yake ya sasa utaelewa ni nini unatakiwa kujifunza kutoka kwake.
Ongelea Ndoto zako;
Watu wengi walioendelea walijua watafika wanapotaka kufika ,Bondia
Maaarufu Duniani Mohamed Ali alisema “I am the greatest, I said that
even before I knew I was.” Alijua yeye ni shujaa hata kabla hajajua
atakuwa, ukifwatilia nyimbo za Drake, nyimbo kama
“Successful,”ameongelea vitu ambavyo atakuja kuwa navyo na alijua si
rahisi ila ilikuwa ndoto, ndoto yake haikuishia hapo kwenye wimbo
“Dreams Money Can Buy” kwenye mstari “Everybody yelled ‘Surprise!,’ I
wasn’t surprised. That’s only because I had been waiting on it.” Anasema
hakuna na mshangaao sababu alikuwa anasubiria hayo, hayo nini
mafanikio.Jambo la kujifunza, ukiwa unajua ndoto zako na mipango yako kimaisha au kibiashara hata siku ukija kufanikiwa hautoona ajabu sababu ulifanya kazi kwa bidii. Tembelea ndoto zako jiamini.
Weka malengo Yako hadharani
usiogope kushindwa, ili siku ukija kufanikiwa wasikuulize ulipita
wapi sababu walishuhudia ukianguka na kunyanyuka mara kadhaa kitu kimoja
kuhusu Drake ni mtu wa ngoma mpya mara kwa mara ndani ya muda si chini
ya miezi 6 Drake alitoa mixtape yake If You’re Reading This It’s Too Late
pamoja na kolabo ya mixtape na future. Kitu nilichogundua ni kwamba
Drake hawaachi fans mda mrefu bila kitu kipya, hii ni nzuri katika
biashara. Sababu hausauliki kirahisi na fans wako. Ukiachilia mbali
ngoma yake mpya ya HOTLINE BRING iliyoleta gumzo mtandaoni baada ya
Drake kucheza staili ya kipekee sana.kitu cha kujifunza biashara inaitaji mzigo mpya mara kwa mara, kuwa mbunifu na kutoishiwa na bidhaa, unachotakiwa kujifunza kutoka kwa Drake ni kutomfanya mteja wako akusahau, hii pia wasanii wa kibongo wanatakiwa wajifunze ili wasipotee katika game.
Fursa na ujue kuitumia
Jambo la kujifunza Drake anajua kutumia fursa, katika kila jambo unalofanya na linalokukuta likiwa baya na ujue jinsi ya kukabiliana nalo, Drake alitumia wakati huo kujiongezea mashabiki na kukuza biashara yake , kwahiyo Drake ni zaidi ya mwanamziki ni mfanyabiashara anejielewaa.
Namba zinaongea.
Japo kuwa kuna wasanii wengine wakubwa marekani lakini Drake ni moja
kati ya waliofanikiwa zaidi , drake ni moja kati ya wasanii 4 kushika
nafasi za juu za Billboard, Drake ameuza zaidi ya kopi million 4
kutoka 2012,hadi sasa. hadi kumshinda mkali wa hiphop Jay-Z. Pia Drake
ni moja kati ya wasanii walio chukua nafasi tatu za juu za kwenye
BillBoard kwa mwaka 2015, Pia Drake ameshika namba tatu kwenye orodha ya
Forbes ya wasanii wa HipHop waliongiza mshiko zaidi ‘Hiphop Cash Kings’Kitu cha kujifunza ni kwamba, haijalishi majina mangapi makubwa yako mbele yako kuna uwezekano wa wewe kufanikiwa tuu, ni kujiamini na kujua nafasi yako cha muhimu ni kujielewa na ujue nini unataka.
No comments:
Post a Comment