Breaking News
recent

Wakati anasherekea kufikisha umri wa miaka 29, Jifunze haya kutoka Drake.

Kuna mambo mengi ya kujifunza kutoka kwa wasanii, ukiachilia mbali ujumbe uliopo ndani ya nyimbo zao, wasanii wa muziki wapo kibiashara sana miaka ya sasa, sababu ya kukua kwa biashara ya muziki duniani kote,
Aubrey Graham  “Drake” alizaliwa  Oktoba 24   kwa jina la kisanii, msanii aliefikia mauzo ya platinamu kwa mwaka 2015, ukiyatazama maisha ya Drake tangia utoto wake na maisha aliyopitia kabla hajawa msanii mkubwa ukitazama  maisha yake ya sasa utaelewa ni nini unatakiwa kujifunza kutoka kwake.

Ongelea Ndoto zako;
Watu wengi walioendelea walijua watafika wanapotaka kufika ,Bondia Maaarufu  Duniani Mohamed Ali alisema “I am the greatest, I said that even before I knew I was.”  Alijua yeye ni shujaa hata kabla hajajua atakuwa, ukifwatilia nyimbo za Drake, nyimbo kama  “Successful,”ameongelea vitu ambavyo atakuja kuwa navyo na alijua si rahisi ila ilikuwa ndoto, ndoto yake haikuishia hapo kwenye wimbo “Dreams Money Can Buy” kwenye mstari “Everybody yelled ‘Surprise!,’ I wasn’t surprised. That’s only because I had been waiting on it.” Anasema hakuna na mshangaao sababu alikuwa anasubiria hayo, hayo  nini mafanikio.
Jambo la kujifunza, ukiwa unajua ndoto zako na mipango yako kimaisha au kibiashara hata siku ukija kufanikiwa hautoona ajabu sababu ulifanya kazi kwa bidii. Tembelea ndoto zako jiamini.

Weka malengo Yako hadharani
usiogope kushindwa, ili siku ukija kufanikiwa wasikuulize ulipita wapi sababu walishuhudia ukianguka na kunyanyuka mara kadhaa kitu kimoja kuhusu Drake ni mtu wa ngoma mpya mara kwa mara  ndani ya muda si chini ya miezi 6 Drake  alitoa  mixtape yake If You’re Reading This It’s Too Late  pamoja na kolabo ya mixtape na future. Kitu nilichogundua ni kwamba Drake hawaachi fans mda mrefu bila kitu kipya, hii ni nzuri katika biashara. Sababu hausauliki kirahisi na fans wako. Ukiachilia mbali ngoma yake mpya ya HOTLINE BRING iliyoleta gumzo mtandaoni baada ya Drake kucheza staili ya kipekee sana.
kitu cha kujifunza biashara inaitaji mzigo mpya mara kwa mara, kuwa mbunifu na kutoishiwa na bidhaa, unachotakiwa kujifunza kutoka kwa Drake ni kutomfanya mteja wako akusahau, hii pia wasanii wa kibongo wanatakiwa wajifunze ili wasipotee katika game.

Fursa na ujue kuitumia
Drake anajua fursa, beef yake na Meek Mill mpenzi wa Nick Minaj, Drake aliitumia vizuri  baada ya Meek Mill kumpaka drake kwamba hajawahi andika nyimbo zake mwenyewe Ndani ya  siku 4 Drake aliachia ngoma ya kumdiss Meek Mill iliitwa “Charged up”  mashabiki walitegemea majibu kutoka kwa  Meek Mill, Hata kabla Meek Mill hajajibu drake alitoa Ngoma nyingine tena baada ya siku Nne “Back to Back” Meek mill alijibu disi akiwa kachelewa sana, mashabiki waliona ushindi kwa Drake na  hiyo ilimuongezea mashabiki lakini mbali ya kushinda mashabiki aliziachia kupitia Apple Music ambao alipata mshiko wa kutosha.
Jambo la kujifunza Drake anajua kutumia fursa, katika kila jambo unalofanya na linalokukuta likiwa baya na ujue jinsi ya kukabiliana nalo, Drake alitumia wakati huo kujiongezea mashabiki na kukuza biashara yake , kwahiyo Drake ni zaidi ya mwanamziki ni mfanyabiashara anejielewaa.

Namba zinaongea.
Japo kuwa kuna wasanii wengine wakubwa marekani lakini Drake ni moja kati ya waliofanikiwa zaidi , drake ni moja kati ya wasanii 4 kushika nafasi  za juu za  Billboard, Drake ameuza zaidi ya kopi  million 4  kutoka 2012,hadi sasa.  hadi kumshinda  mkali wa hiphop Jay-Z. Pia Drake ni  moja kati ya wasanii walio chukua nafasi tatu za juu za kwenye BillBoard kwa mwaka 2015, Pia Drake ameshika namba tatu kwenye orodha ya Forbes ya wasanii wa HipHop waliongiza mshiko zaidi ‘Hiphop Cash Kings’
Kitu cha kujifunza ni kwamba, haijalishi majina mangapi makubwa yako mbele yako kuna uwezekano wa wewe kufanikiwa tuu, ni kujiamini na kujua nafasi yako cha muhimu ni kujielewa na ujue nini unataka.
ABC

ABC

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.