Breaking News
recent

Je, mnaweza kubaki marafiki wewe na mpenzi wako baada ya kuachana?

Swali gumu? Ndio najua sio rahisi lakini kama uliachana na mpenzi wako bila ugomvi sidhani kama ni vibaya mkiwa tu marafiki kama inawezekana, wapo wanaosema haiwezekani na inategemea, unaweza kijiuliza  sababu ya nyie wawili kushindwa kuendelea kuwa wapenzi ni nini?  Ila upo uwezekano wa nyie wawili kuwa marafiki lakini kuna mambo muhimu  ya kuzingatia.
Je ni kweli mnataka kuwa marafiki?
Jaribu kujiuliza kama kuna ulazima wa wewe na yeye kuwa marafiki, na mtaweza kuvumilia mipaka ya urafiki, kumbuka hamuwezi kuwa marafiki kama marafiki wengine, tayari mmepitia mahusiano mnafahamiana zaidi ya urafiki,  kuwa makini kabla hujaamua kuanza urafiki huo mpya.
Una uhakika na hisia zako?
Upo wakati unaachana na mtu sababu tu, kuna mambo mengi yalisababisha mahusiano hayo kuisha, je bado unahisia za mapenzi na mtu huyo, na unadhani utaweza vumilia nyie kuwa marafiki tu, kama huwezi na unahitaji kuendelea  na maisha yako ni vizuri ukapingana na swala la nyie kuwa marafiki sababu urafiki huo hautadumu.
Jichanganye nae katika Vikundi.

Mkiwa katika kundi la marafiki, ni salama zaidi hasa kama mna marafiki wa aina moja, marafiki zako na marafiki zake pamoja, kutoka chuoni au Darasa moja ,
Bado una Wivu nae?
Kama bado unajisikia vibaya ukimuona na mtu mwingine na ni wazi bado unampenda, na ni vizuri kama utakaa nae mbali,na kama yeye anaona wivu ukiwa na mtu mwingine basi si sawa mkiendelea kuwa marafiki sababu bado mnahitaji kuwa zaidi ya marafiki.
Bado Mnakumbuka mlipotoka?
Mnapokumbuka mambo mliyofanya pamoja, kama mitoko ya pamoja kwenye sherehe mbalimbali,matamasha  mlienda pamoja na vitu vingine vyote ambavyo vinabeba kumbukumbu yenu si vizuri kuviongelea kama mmeamua kuwa marafiki,  si vizuri kuongelea mliyoamua kuyaacha, mnaweza mkarudi nyuma mlipotoka.
Vitu muhimu vya kuzingatia ni, kujiuliza kama mlishindwa kuwa wapenzi kwanini muwe marafiki  sasa na kwanini?  Kitu cha muhimu ni kuendelea na maisha sababu maisha hubadilika na watu hubadilika pia
ABC

ABC

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.