Breaking News
recent

Jay Z ashinda Kesi ya haki miliki ya wimbo wake wa ‘Big Pimpin’

Jay Z na producer wa wimbo wa ‘Big Pimpin’ uliotoka mwaka 1999, Timbaland  wameshinda kesi iliyokua inawakabili kuhusiana haki miliki ya wimbo huo.

Kesi hiyo ilifunguliwa na Osama Ahmed Fahmy ambaye ni binamu wa Baligh Hamdi wa Misri kwa madai ya kuwa vionjo vya wimbo wa binamu yake wa mwaka 1957, ‘Khosara khosara’ vilitumika kwenye wimbo huo wa Jay Z ‘Big pimpin’.
Jaji aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo Christina A. Snyder ametupilia mbali kesi hiyo  baada ya kusikiliza ushahidi kutoka kwa wataalam wa sheria wa Misri, Hata hivyo upande wa walalamikaji umeonesha kutoridhishwa na uamuzi wa jaji na wamesema watakata rufaa.

ABC

ABC

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.