Breaking News
recent

Umewahi kujiuliza kwanini watu wanaita Mafua ugonjwa wa mapenzi?

Ukiacha Mafua,Umeshawahi kufikiria, mchango wa tendo la ndoa katika afya yako, kabla sijakuambia umuhimu wake, usidhani kuwa tendo la ndoa linatibu Malaria, muone daktari pale unapojisikia mgonjwa, yapo mambo kadhaa husaidia afya yako kwa kila tendo moja la ndoa. Hizi ni sababu 7 muhimu unapata  baada ya tendo la ndoa.
  1. Hupungua wingi wa Kalori
Wakati wa tendo la ndoa moyo unaweza kusukuma damu kwa kiasi kikubwa kuliko kawaida hii husaidia kupunguza kalori ama mafuta katika moyo, kwa dakika 30 mwili unauwezo wa kupunguza kalori 85 hadi 200,kama unafanya tendo la ndoa nusu saa kila siku una uwezo wa kupunguza kilo 4.5 kwa mwaka.
  1. Ukakamavu wa Mifupa na Misuli
Tendo husaidia uzalishwaji wa homoni ya testeroni ambayo inasaidia misuli na mifupa pia husaidia nguvu ya mwili, na kukupa hamu ya tendo, kupungua kwa homini ya testeroni husababisha uchovu, kutokuwa  hamu na tendo la ndoa na msongo wa mawazo.
  1. Hupunguza uwezekano wa kupata Kansa Ya kibofu
wanaume wanaoweza kupungua manii mwilini mwao mara kwa mara wana uwezo wa kupunguza uwezekano wa kupata kansa kwa asilimia 30. Kutoa manii kwa mwanaume inaweza ikawa kwa tendo la ndoa ama kwa kujichua japo haishauriwi kujichua.
  1. Muhimu kwa Moyo
Utafiti kutoka Chuo cha Queen Marekani, unaonyesha wanaume wanaoshiriki  tendo mara 3 kwa wiki wanapunguza uwezekano wa kupata ugonjwa wa moyo na kiarusi kwa asilimia 50. Pia husaidia kupunguza uwezekano wa kupata shinikizo la damu.
  1. Hupunguza Msongo wa mawazo (Stress)
Tafiti mbalimbali zimeonyesha,kuna watu wengi baada ya tendo  huwa wamepunguza msongo  wa mawazo,  kwa kiasi kibubwa.
  1. Kusaidia kinga ya Mwili.
Kuna usemi, mafua ni ugonjwa wa mapenzi , hii ni kwa sababu Kinga yako ya mwili huongezeka kwa kushiriki tendo mara kwa mara, hii ni kwa sababu mzunguko wako wa damu kufanya kazi vizuri,kupumua vizuri na sababu ni moja kati ya zoezi ni rahisi kukusaidia kufungua pua kama ulipata mafua na kukufanya uweze kupumua vizuri .
  1. Usingizi wako Muhimu
Unapata tatizo la kukosa usingizi? Inaweza sababishwa na msongo wa mawazo na mambo mengine mengi. Umewahi kujiuliza kwanini watu wanalala baada ya tendo, hii ni kwa sababu mwili kwa ujumla unapata kupumzika (relaxed)  baada ya tendo, kemikali inayoitwa serotonini  huongezeka mwilini na kumfanya mtu awe na furaha.

Kwakua hukuyajua haya na Wakati unawaza kukutana na mwenza wako, ni vizuri kuzingatia afya zenu, kwa kuhakikisha wote ni salama, ninapo ongelea usalama wa afya wengi wetu wanawaza maambukizi ya ukimwi pekeake, kuna magonjwa ya zinaa ambayo ni hatari  zaidi basi ni vuzuri kabla hamjarukiana mkapima au mtumie kinga.
ABC

ABC

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.