Breaking News
recent

Vanessa Mdee amesema msanii kushinda Tuzo nyingi haimaanishi kuwa anafanya vizuri sana

Mshindi wa Tuzo ya Afrimma ‘Best Female East Africa’ Vanessa Mdee amesema msanii kushinda Tuzo nyingi haimaanishi kuwa anafanya vizuri sana.
Vee Money ameyasema hayo wakati anafanya mahojiano na kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio ambapo alimtolea mfano Wizkid, Alisema
“Msanii kuwa na Tuzo, kwa mfano tumuangalia WizKid ana tuzo chache, lakini muziki wake unafanya vizuri dunia nzima, Drake anamtafuta, Swizbeat anamtafuta, Alicia Keys ana mtafuta na ratiba yake iko busy mwaka mzima, So haijalishi”
Katika hatua nyingine Vee alielezea experience aliyoipata kufanya kazi na 2face Idibia kwenye Coke Studio  “Tulivyokuwa tunashoot nilikuwa na 2face, wengine walikuwa hawajafika, sijawahi kufanya kazi na msanii mkubwa kama yeye, ana heshimu kazi, nimejifunza kitu toka kwake mkarimu, na kuna nafasi kubwa kwa wasanii wa Afrika kufika mbali" alisema mwimbaji huyo wa Never Ever.
ABC

ABC

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.