Breaking News
recent

Maneno ya Barack Obama kwa Rapper Kanye West kuhusu kuwania Urais 2020.....

Hivi karibuni rapper wa Marekani Kanye West alitangaza nia yake ya kutaka kuingia ikulu ya Marekani katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka 2020.
Kanye alitangaza nia yake hiyo wakati wa tuzo za VMAs 2015.
Rais wa Marekani Barack Obama amemshauri rapper huyo kuhusu uamuzi wake huo wakati waalipohudhuria hafla ya uchangishaji fedha huko San Francisco iliyofanyika jana Oktoba 10 wakati Kanye West naye akiwa mmoja wa waliohudhuria.
Kwanza Obama alishangazwa na uamuzi wa Kanye West kuwania nafasi hiyo na pia hakuwa na kikubwa cha kumshauri kuhusu uamuzi wake huo.
Amemtaka kama Rais atumie muda mwingi kufanya maamuzi kwa sababu kuna watu wengi ambao wana tabia za ajabu hivyo anapaswa kukabaliana nao ili aweze kumudu nafasi yake.
Pia alimuuliza kama anafikiri tena Wamarekani watampa Mmarekani mweusi nafasi ya kuwaongoza kama ilivyokuwa kwake.
Obama na Kanye West wote wametokea katika jimbo la Chicago Kusini.

Hii ni Video wakati akizungumza….CLICK HERE TO VIEW THE VIDEO

ABC

ABC

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.