Breaking News
recent

Maneno ya Nicki Minaj kuhusu Drake & Meek Mill + beef yake na Miley Cyrus!


First lady wa label ya Cash Money Records Nicki Minaj ameingia kwenye headlines za burudani baada ya interview yake na jarida la The New York Times Magazine, miongoni mwa majarida makubwa ya mastaa wa kike wa HipHop Marekani.


Akiwa kwenye interview na jarida hilo Nicki Minaj alizungumzia vitu vingi baadhi vikiwa mtazamo wake kuhusu beef ya Drake na mpenzi wake Meek Mill pamoja na beef yake na Miley Cyrus msanii wa Pop nchini Marekani... kwenye mazugumzo Nicki alikuwa na haya yakusema kuhusu Miley Cyrus..
>>> ” kitendo cha yeye kukasirishwa na nilichokisema kuhusu kitu kinachowagusa wanawake weusi kinanifanya nimchukulie tofauti. Yeye kila siku yupo kwenye videos na watu weusi haswa wanaume na mara nyingi anawaaakila wasanii wa weusi wa kike kwenye majukwa yake tofauti, lakini eti hutaki kujua wanawake weusi wanajisikia vipi kuhusu vitu muhimu vinavywagusa (kama ile tuzo)!? Sio kweli, huwezi kutaka mazuri tu kuhusu sisi bila kupenda au kuelewa mabaya yanayotuzunguka. kama anapenda kuenjoy lifestyle yetu na kuwa karibu na sisi, kuimba na kuperform na sisi basi inabidi ajue yale mambo yanayotugusa na kutuumiza pia, na sio tofauti!” <<< Nicki Minaj.


Nicki Minaj: (NY Times Magazine Photo Shoot)
Na alipoulizwa kuhusu beef ya Meek Mill na Drake, Nicki Minaj alikuwa na haya ya kusema…
>>> “Wale ni watu wazima, watu wazima wenye akili zao timamu… hii issue ni kati yao wawili wao ndio wanajua wanaipeleka wapi hii beef… ila binafsi siipendi, sijiskii vizuri kuwaona wakiwa hivyo, na siku zote maamuzi ya busara ni kutokuchagua upande haswa issue ikiwa inawahusu watu wawili unaowapenda. Kwanza ni ujinga. Nataka tu yaishe soon.” <<< Nicki Minaj.


ABC

ABC

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.