Mshambuliaji wa Real Madrid Christiano Ronaldo ameingia tena kwenye headlines za michezo baada ya jana kufanikiwa kuhitimisha mabao 500 kufuatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Malmo FF ikiwa ugenini.Idadi hiyo inamfanya mshambuliaji huyo staa kufikia rekodi ya gwiji wa soka wa Real Raul aliyekuwa akiongoza kwa kuifungia klabu hiyo magoli mengi.Staa ambaye ni mchezaji bora wa dunia alifunga mabao hayo katika dakika ya 29 na 90 Uwanja wa Swedbank katika mchezo wa Kundi A.Ronaldo amefikisha mabao 82 katika Ligi ya Mabingwa na kuhitimisha idadi ya mabao 501 tangu aanze kucheza soka
No comments:
Post a Comment