Breaking News
recent

Khloé Kardashian na Lamar Odom waifuta kesi ya Talaka, kuendelea kuwa Mume na Mke.

Ndoa ya mcheza kikapu wa NBA Lamar Odom na Khloé Kardashian iliyokua kwenye mawe imepona kufuatia kuugua kwa mcheza kikapu huyo, imeripotiwa kuwa wanandoa hao wameifuta kesi ya talaka ya ndoa yao.
Siku moja baada ya  Khloé kumpiga chini aliyekuwa mpenzi wake wa sasa James Harden ili kupata muda wa kumuuguza Lamar Odom wawili hao waliofunga ndoa mwaka 2009 japo ilivunjika baada ya miaka minne wameamua kuendelea kuwa mume na mke.
Kwa mujibu wa TMZ, mwanasheria wa  Khloé aitwaye Laura Wasser , Siku ya Jumatano (Oct. 20) alienda kwa hakimu kuomba kusitisha kesi hiyo huku wote wakiwa wamesaini hati ya kukubali kufuta kesi ya kuvunja ndoa yao, na jaji alifanya kama walivyoomba.
Khloé alifungua kesi hiyo ya kudai talaka mwezi December mwaka 2013.

ABC

ABC

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.