Breaking News
recent

Cristiano Ronaldo katwaa kiatu cha nne cha dhahabu na kuweka rekodi.

 Mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno na klabu ya Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo ameingia tena katika headlines baada ya kutwaa tuzo nyingine ya ufungaji bora. Cristiano Ronaldo ambaye September 30 aliweka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa klabu ya Real Madrid kwa kufunga jumla ya goli 324 na kuvunja rekodi iliyokuwa inashikiliwa na Raul Gonzalez.
 October 13 Cristiano Ronaldo alipokea kiatu cha dhahabu baada ya kuibuka mfungaji bora wa Ulaya kwa kufunga magoli mengi katika mechi zinazochezwa ndani ya nchi husika kwa kufunga jumla ya goli 48 katika mechi 35. Ronaldo amechukua kiatu cha dhahabu cha tatu akiwa na Real Madrid baada ya mara ya kwanza kutwaa tuzo hiyo akiwa Man United msimu wa 2007/2008.
 Kwa ujumla Ronaldo anaweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kutwaa tuzo hiyo mara nne, huenda ukawa unajiuliza namna au mfumo unaotumika kutoa tuzo hiyo, tuzo hii ushirikisha wachezaji wanaotokea katika Ligi kubwa kama Ligi Kuu Uingereza au Hispania hata kama watafunga magoli machache kuliko wachezaji wanaotoka Ligi dhaifu wanaweza kutwaa tuzo hiyo.


ABC

ABC

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.