Breaking News
recent

Baada ya Wenger kuponda uamuzi wa Liverpool, Ferguson azungumzia uwezo wa Jurgen Klopp...


Stori bado katika headlines za michezo Uingereza ni kuhusu Liverpool kumtimua Brendan Rodgers na kumpa nafasi kocha wa Kijerumani Jurgen Klopp ambaye anatajwa kuwa kocha wa 20 aliyewahi kujiunga na klabu hiyo na wa kwanza wa Kijerumani kupata nafasi katika timu hiyo, lakini ni kocha wa pili wa Kijerumani kufundisha timu za Ligi Kuu Uingereza.
October 9 kocha wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger alitoa maoni yake kuhusu maamuzi ya Liverpool kumfuta kazi Brendan Rodgers kwa upande wake aliona hawakufanya maamuzi sahihi, Wenger alizungumzia upande wa Liverpool kumfuta kazi kocha huyo lakini hakumgusa kocha mpya aliyerithi nafasi Jurgen Klopp kuhusu uwezo wake.
Jurgen Klopp wakati wa utambulisho Liverpool

October 10 aliyekuwa kocha wa klabu ya Manchester United aliyodumu nayo katika kipindi cha zaidi ya miaka 2o Sir Alex Ferguson amezungumza kwa upande wa uwezo wa Jurgen Klopp. Ferguson amekiri kumfahamu vizuri Jurgen Klopp na anakubali uwezo wake anaamini Liverpool wamefanya uamuzi sahihi kumchukua kocha huyo.
“Vizuri ni maamuzi sahihi namkubali Jurgen Klopp, nilimfahamu vizuri kocha huyo tulipokuwa Geneva Uswiss katika mkutano wa makocha, ni kocha mzuri uwezo wake unatambulika alipokuwa Dortmund, Sikupenda kusema hivyo kwa sababu naogopa kiasi, ila naamini  Liverpool atafanya vizuri”

ABC

ABC

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.