Breaking News
recent

Unapenda kupiga Selfie? haya ni mambo ya kuzingatia wakati wa kupiga selfie..

Selfie sio msemo mpya kwa watu wengi, upigaji huu wa picha umekuwa maarufu kwa watu wengi hasa kwenye mitandao ya kijamii duniani kote, hakuna kanuni za kupiga selfie wala sheria  ila kuna mambo machache ya kuzingatia ukichukua selfie.
  1. Selfie sio Photoshop: usiwaze kuhusu ubora wa muonekano wako, uwe na muonekana wa asili (natural), selfie ukiwa umetoka kuamka au ukiwa na kikombe cha chai mezani si lazima kujipamba ili uonekane mrembo/mtanashati zaidi
  1. Mwanga: picha nzuri ni mwanga mzuri, selfie nzuri ni zile zinazopigwa nje zaidi kuliko ndani, mwanga mwingi sana au mdogo sana unaweza fanya picha iwe ina mwanga sana au iwe na giza sana mda mzuri wa selfie ni asubuhi na jioni kabla jua halijazama.
  1. Usikunje midomo yako: maarufu kama “duck face” watu wengi hasa wadada wanapenda sana staili ya kukunja midomo yao, sura yako haitoonekana kiasili (natural)
  1. Selfie Bafuni: vioo vya mabafu ndio sehemu za selfie kwa baadhi ya watu, kupiga picha kwenye vioo vya bafuni katika hotel au migahawa mikubwa si poa, selfie bomba haipigwi maliwatoni.
  1. Usidanganye kulala kwenye selfie:  Hii watu hupiga waonekane kama kuna mtu mwingine kapiga hiyo picha kitu ambacho si kweli, haumdanganyi mtu linapokuja swala la selfie , mikono yako, pozi lako ni ishara tosha kwamba umejipiga picha mwenyewe.
  1. Kuwa wa tofauti: badilisha sehemu unazopiga picha kila siku, chumbani, ofisini, barabarani zinaweza kuwa ni sehemu za kila siku, selfie chini ya maji ukiwa ufukweni juu ya majengo marefu, ila uwe makini na usalama wako.
  1. Background: kuwa makini na sehemu uliyochagua na nini kitaonekana nyuma  yako, mfano nguo nyuma ya mlango, wako au chumba kisicho na mpangilio mzuri  picha moja anaweza ikakuvunjia heshima ama kuwapa nafasi ya watu  kukuelewa vibaya.
ABC

ABC

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.