Breaking News
recent

Kumsaidia Msanii chipukizi sio kumpeleka studio tu kama wengi wanavyofikiri – Izzo Bizness.

 Izzo Business ameweka wazi kuwa kwa nafasi yake, anasaidia kunyanyua vipaji vya wasanii wanaochipukia kwa kutenga muda wake kutoa ushauri kama ambavyo binafsi ameweza kufanikiwa kwa kuzingatia mawazo na kujifunza kutoka kwa wasanii waliomtangulia.
Akiongea na East Africa Radio, Izzo alijitolea mfano yeye mwenye , Alisema

“Mimi mara nyingi sijafikia uwezo wa kuwachukua watu kuwasaidia kuwapeleka studio, kuwalipia video na nini, lakini kwa mtu ambaye naona ana nia na malengo kwasababu hata mimi nilifight, walikuwepo kina Sugu kina nani ambao walikuwepo juu yangu, wakina adili, kikubwa ambacho nilikua nachukua kwao ni mawazo na kuangalia ambacho walikua wanafanya”

Pia Izzo ameeleza kwa wasanii wenye malengo ya kukua na vipaji ndani yao, huwa anachukua nafasi ya kuwajenga wawe wasanii bora wa baadaye, ushauri wake wa wazi kwao pembeni ya muziki ukiwa ni displine, heshima kwa kila mtu na kuzingatia muda.


ABC

ABC

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.