Breaking News
recent

Diamond apanga kufanya video ya collabo yake na Ne-yo Afrika na Marekani.

Staa wa Bongo Fleva na mshindi wa Tuzo ya MTV EMA ‘Best Worldwide act Africa/India’ Diamond Platnumz ameelezea mpango wake wa kufanya video kali ya wimbo aliomshirikisha staa wa Marekani Ne-yo, amesema anapanga kuifanya baadhi ya sehemu za Afrika na Marekani.
Akizungumza na Mzazi Willy Tuva, Diamond amesema Collabo hiyo imeshakamilika lakini hawezi kusema utatoka lini kwasababu kuna mambo anamalizia.
“Collabo tayari imeshakamilika tuko kwenye process za kumalizia vitu vitu fulani ili iweze kuachiwa ila siwezi sema haswa itaachiwa lini lakini haitakuwa na muda mrefu, kwasababu unapotoa nyimbo ni lazima niangalie nyumba maana sasa hivi Tanzania kuna uchaguzi” Alisema Diamond
Pia Diamond ameelezea kuwa ana project nyingi ameziandaa kwa ajili ya mashabiki wake na kuonesha dunia kuwa watanzania wanaweza.
ABC

ABC

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.