Ni kawaida kwa siku za hivi karibuni
kuona watu fulani kutoka tasnia fulani kupewa tuzo za heshima kwa
kutambua mchango wao katika sekta husika. Chama cha waandishi wa habari
za michezo Tanzania TASWA, kimetangaza rasmi kufanyika kwa tuzo hizo Jumatatu ya October 12 huku mgeni rasmi akiwa Dk Jakaya Mrisho Kikwete.
Tuzo hizo ambazo hufanyika kila mwaka kwa mwaka huu zitakuwa tofauti kidogo kwani zitatumika kumuaga Rais Jakaya Kikwete na kumpa tuzo ya heshima kwa kuthamini mchango wake katika kipindi cha miaka 10 aliyokuwa madarakani.
Awali tuzo hizo zilikuwa zifanyike
October 8 ila kwa sasa zitafanyika Jumatatu ya October 12, tuzo
zitatolewa kwa wanamichezo waliofanya vizuri katika kipindi cha miaka
10, baadhi ya tuzo zitakazotolewa siku hiyo ni tuzo 10 za wachezaji bora
waliofanya vizuri katika kipindi cha miaka 10, tuzo 5 kwa viongozi wa
michezo, taasisi iliyochangia kukuza michezo katika kipindi cha miaka 10
na tuzo ya heshima kwa Mh Rais.
Mwewnyekiti wa TASWA Juma Pinto na katibu mkuu wa TASWA Amir Mhando wamethibitisha hayo kufanyika katika mkutano na waandishi wa habari.
“kwa
wale ambao hamfahamu tutatoa Tuzo kumi kwa wachezaji wale ambao
wamefanya vizuri katika kipindi cha miaka kumi ila tumeangalia nje ya
Tanzania yaani Afrika Mashariki lakini tutatoa tuzo kwa viongozi watano
waliochangia kukuza michezo, tuzo zote hizo zitatolewa na Rais
Kikwete”>>> Amir Mhando

No comments:
Post a Comment