Breaking News
recent

Kijana aliyetengeneza saa ya akutani marekani akutana na raisi Omar Al-Bashir.

Mvulana wa umri wa miaka 14 nchini Marekani, aliyegonga vichwa vya habari baada ya kukamatwa kwa kupeleka saa ya kujitengenezea shuleni, amekutana na Rais wa Sudan Omar al-Bashir.
Ahmed Mohamed na familia yake walilakiwa katika ikulu ya rais katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum Jumatano, kwa mujibu wa kituo cha redio cha serikali.
Mvulana huyo alifurushwa darasani na kutiwa pingu baada ya mwalimu wake kudhani saa hiyo ilikuwa bomu.
Kukamatwa kwake kulishutumiwa sana. Polisi hawakumfungulia mashtaka yoyote.
Babake mvulana huyo, Mohamed Hassan al-Sufi, ni mhamiaji kutoka Sudan anayeishi Marekani.
ABC

ABC

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.