“Ingekuwa kweli nyimbo ya Harmonize ambaye ndio msanii wa Diamond, ingekuwa Exclusive MTV au ingekuwa inapigwa kila siku kwasababu ndio biashara yake, si ndio, hilo sio neno la kweli, yule aliyetoa hiyo habari amechukua kichwa cha habari na kukinya habari kwa watu wengine” Babu Tale aliiambia XXL ya Clouds Fm.
“Diamond alihojiwa, alikuwainterview kwenye.. moja ya swali aliloulizwa wasanii gani ambao umewasaidia, na je, unasupport mziki wa nyumbani kwenda nje? yeye akajibu mbona mimi nasaidia watu wengi na kuna kipindi huwa napigiwa simu mtu anauliza labda unamjua fulani mzuri? kuna vipindi, media za nje huwa zinanipigia unamjua fulani mzuri? me nawaambia mzuri kwasababu ya kutengeneza mazingira watu wote tutoke tutangaze mziki wetu nje, alieandika kile kichwa cha habari akasema kwamba Diamond ndiye anayeamua myimbo fulani kwenda sehemu fulani kitu ambacho siyo cha kweli, kama Diamond angekuwa anaamuahivyo maana yake hayo maamuzi anafanya na menejimenti basi nyimbo zote za sijuhi TMK, za TipTop, za mkubwa na wanawe za watu wote wa karibu na Diamond wote ndio zingekuwa zinapigwa sana kuliko hata wengine” Babu Tale aliongeza.
Diamond alifanya Mahojiano na kipindi cha Papaso cha TBC Fm, ambapo alisema
“Nikiamua kubana mbona naweza tu, kwasababu vituo vingi vya nje vinanisikiliza kwa mfano tu MTV wenyewe wakipokea video ya msanii yeyote kutoka hapa (Tanzania) wananipigia wananiuliza kwanza huyu vipi? Tuicheze ngoma yake au? Mimi huwa nasema anafanya vizuri huku, basi inapita wanaicheza nikiamua kubana si naweza tu.” Pia muimbaji huyo wa ‘Utanipenda’ alisema yeye na uongozi wake waliwashawishi kituo cha SoundCity Tv ya Nigeria kuanzisha kipindi cha Top Ten East ambacho huonesha chati ya video za wasanii wa Afrika mashariki, na kuongeza kuwa walizungumza pia na MTV Base kuanzisha kipindi kama hicho, Tazama Interview hiyo hapo juu.
No comments:
Post a Comment