Katika hotuba yake iliyojaa kila
aina ya hisia kali, Rais Obama amebainisha wazi mipango yake juu ya
kuweka mikakati thabiti ya udhibiti silaha za moto, akisema kwamba
Marekani haipaswi kukubali mauaji kama gharama yoyote.
Obama amesema kwamba hatua madhubuti zinapaswa kuchukuliwa ambazo
zitajumuisha ufuatiliaji wa tangu awali wa upatikanaji silaha, pia
uchunguzi wa afya ya akili utazingatiwa na hii ni pamoja na kumbukumbu
za uhalifu wa mtuhumiwa zitahusishwa pia.Rais Obama anatarajiwa kuweka hadharani hatua zitakazochukuliwa dhidi ya matumizi mabaya ya silaha na hasa ikizingatiwa hii ni miaka ya upinzani mkali katika serikali yake.
Hata hivyo chama cha wauza silaha nchini Marekani kimekosoa hotuba ya Rais na kusema kwamba mapendekezo yake hayatazuia mauaji ya halaiki kutokana na aliyoyasema katika hotuba yake.
No comments:
Post a Comment