Wasanii wa Nigeria, Don Jazzy na Olamide wamepatana baada kurushiana
maneno makali kwenye Tuzo za The Headies 2015 zilizofanyika mwishoni mwa
wiki iliyopita.
Don Jazzy na Olamide wote wameweka picha moja na ujumbe mmoja kwenye
mitandao ya kijamii kuwaonesha mashabiki wao kuwa wamemaliza tofauti
zao, wameandika
“We are very sorry for the wahala. Make una no vex ooo.
It is our responsibility to lead but then again we re only human and we
all make mistakes. #WeAreSorryHeadies #WeAreSorryFans #PeaceAndUnity
#YBNL #SMD #OneLagos #OneNigeria”
Ugomvi wa wasanii hao nguli wa Naija ulianza siku ya Utoaji wa Tuzo
za The Headies baada Reekado Banks, aliye chini ya Mavin Records ya Don
Jazzy kumshinda msanii aliye kwenye lebo moja na Olamide, Lil Kesh na
kushinda tuzo ya ‘The Next Rated Award.’ ambayo ilikua inakuja pamoja na
zawadi ya gari aina ya Hyundai suv.
Olamide Alipopanda jukwaani akiwa na crew nzima YBNL aliamua
kufunguka ya moyoni baada ya msanii wake Adekunle Gold kushinda tuzo ya
Best Alternative akipondea ushindi wa Reekado Banks akidai kuwa Tuzo
hiyo alistahili kupata Lil Kesh
“This award belongs to Lil Kesh. Lil Kesh is our own Next
Rated artist. F**k that shit! The streets ti take over. Every f**king
single was a hit back to back. From lyrically to Shoki to Efejoku. Ko ni
dafun Iya anybody”, alisema Olamide, kutupa mic chini na kuondoka.
Don Jazzy aliyeshinda tuzo ya “Lifetime Achievement Award” alimjibu
Olamide kwa kumuambia kama anataka gari la ushindi wa tuzo
aliyoilalamika anaruhusiwa kwenda kuichukua.
“Egbon Olamide, if you want the car, come and take it,” alisema, Tazama Video ya Drama nzima hapo chini
World Of Pl@tnumz
Music Stories
Don Jazzy na Olamide wapatana baada ya kurushiana maneno makali kwenye Tuzo za The Headies....
ABC
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment