Breaking News
recent

Mahakama kuu yatupilia mbali kesi dhidi ya Mbuge wa Mikumi, Joseph Haule

Mahakama kuu kanda ya Dar es salaam imetupilia mbali kesi iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa ubunge jimbo la Mikumi mkoani Morogoro Bw Jonas Nkya wa (CCM ) dhidi ya Mbunge Joseph Haule kuhusu kuomba kupunguziwa gharama za uendeshaji wa kesi kutoka milioni 15 hadi milioni 1.5.
Kupitia Instagram, Joseph Haule ameandika
“Breaking News: Mahakama Kuu kupitia Mheshimiwa Jaji IGNAS KITUTSI asubuhi hii imetupilia mbali Maombi Madogo ya Kesi ya kuomba kupunguziwa gharama za dhamana ya kesi (security for cost) iliyofunguliwa dhidi yangu na mpinzani wangu Jonas Nkya. Mahakama kuu imetupilia mbali kesi hiyo na kukubaliana na hoja za mapingamizi ya kisheria yaliyowekwa na jopo la Mawakili wangu wasomi linaloongozwa na Tundu Lissu na John Mallya. Mahakama pia imemuamuru mlalamikaji atulipe gharama zetu zote za kesi na usumbufu!!!
ASANTE MUNGU, UKWELI UNA TABIA YA KUSHINDA!!”
Kesi hiyo imetupiliwa mbali na Jaji wa mahakama hiyo Ignas Kitusi kwakuwa vielelezo vilivyofungua kesi hiyo havikukidhi vigezo pia fedha ambazo zilitakiwa kulipwa na mlalamikaji kiasi cha milioni 15 hazikupatikana ndiyo sababu ya kufuta kesi hiyo na jaji kumtaka mlalamikaji kwanza kulipa gharama za usumbufu za kesi hiyo na kama hakuridhika na uamuzi huo akate rufaa.
ABC

ABC

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.