Breaking News
recent

Simshauri mtu yoyote achore tattoo ya Mpenzi wake – Shilole!

Shilole hataki kusikia tena habari za kuchorana Tattoo.
Mwanamuziki huyo amesema hamshauri mtu yeyote achore tattoo kwa sababu ya mapenzi kwasababu watakapoachana haitaleta maana tena
“Sina tattoo tena nimeamua tu kuifuta,tutapendana tu kama ni mapenzi tutapeana ya rohoni,mambo ya kuchorana tattoo nimeshaacha,nishaona hakuna sababu ya kuchora unaweza kuchora tattoo ukazuia mambo yako mengi yanayopita” Amesema Shilole.
Pia ameelezea sababu ya kufuta Tattoo ya Mpenzi wake Nuh anayedaiwa kuachana nae
“Nimeona mwenyewe madhara yake kwahiyo simshauri mtu achore tattoo kwa ajili ya mapenzi nimeamua kufuta tattoo niliyomchora Nuh kwa sababu haina sababu ya kukaa kwenye mwili wangu” Alisisitiza shilole.
ABC

ABC

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.