Baada ya kutengeneza mamilioni ya pesa kwenye biashara ya muziki rapper Snoop Dogg aliona bora awekeze kwenye vitu tofauti kidogo na biashara ya muziki na kujiunga na biashara ya mitandao… kipya kuhusu Snoop Dogg wiki hii ni yeye kutangaza biashara yake mpya kabisa ‘MerryJane’ ambayo huduma zake zitakuwa zinawalenga wale wote ambao ni watumiaji wa bangi aina ya Marijuana!
Kwenye press conference ya TechCrunch Disrupt, San Francisco Snoop Doggalitangaza ujio wa kampuni hiyo ambayo yenywe unaambiwa itakuwa inajihusisha na bangi ya Marijuana tu, na kila kitu kuhusu utumiaji wa bangi hiyo, namna ya kupika chakula kwa kutumia marijuana na namna ya kuenjoy uvutaji wake bila shida yoyote ile! Yeye anaiita “Encyclopedia of Marijuana” yani “Muongozo wa Marijuana!”
Snoop Dogg anasema ameona kuna kitu kimepungua kwenye soko la Marijuana haswa kwa wale watumiaji wa bangi hiyo, yeye ameona kuwa kuna watumiaji wengi sana wa bangi hiyo Marekani lakini hawajui namna ya kuitumia bangi hiyo vizuri, wanakosa ushauri wa kina wa jinsi ya kuitumia bangi hiyo, wanakosa pia ushuhuda wa raha ya bangi hiyo kutoka kwa watu mbalimbali!
>>> “Sisi tunakuja kuwa mtandao wa habari kali za starehe za Marijuana, manake kila mtu anazungumzia athari tu ila wanasahau ina starehe yake pia… sasa hilo ndio shimo ambalo mimi na watu wangu tutakuja kuziba kuwanzia mwezi October! Msijali ni mambo mazuri tu yanakuja, msiogope!” <<< Snoop Dogg.
Website hiyo mpya itakayoaanza mwezi October itakuwa na vitu vingi ikiwemo watumiaji 420 kwa siku, habari chanya kuhusu Marijuana, videos pia na interviews mbalimbali kuhusiana na bangi hiyo na watumiaji wake! Nia yao?… kukuza biashara ya Marijuanakwenye majimbo ambayo matumizi ya bangi hiyo Marekani ni halali kabisa!
Nimekusogezea video inayoelezea mpango huu wa Rapper Snoop Dogg na moja ya video ambayo itakuwa inapatikana kwenye website mpya ya Snoop DoggMerryJane.com hivi karibuni… kipande kinaitwa “Deflowered with the Marines”
No comments:
Post a Comment