Dully Sykes ni Mkongwe wa Bongo Fleva, japo wapo Mastaa wengine pamoja na wakongwe kama yeye ambao wamejiingiza kwenye Siasa kwa kuwapigia Kampeni Wagombea wa nafasi mbalimbali… Dully aliandika kwenye ukurasa wake Instagram kwamba hana Chama na hapendezwi na ishu ya lugha chafu kutumiwa na Makada na Wagombea kuchafuana kwenye Majukwaa ya Siasa.
Kwenye Exclusive Interview Dully kaongea na haya kuhusu msimamo wake >>> “Hiki ni kipindi ambacho wasanii wengi wanatumika kufanya Kampeni, msanii anaweza kuwa na Chama alafu Chama kingine kikamhitaji kwa dau kubwa zaidi, anakosa msimamo…“
“Mwisho wa yote amini unachokiamini na muamimi unayemuamini ila tupige kura kwa amani tarehe 25 October.. nitakuwepo mmoja kati ya watakaopiga kura.” >>> Dully Sykes.
No comments:
Post a Comment