Kocha wa klabu ya Chelsea
ambaye amekuwa akiingia katika headlines mara kadhaa kutokana na tabia
yake ya kupenda kulumbana na kuwatoa mchezoni wapinzani wake kwa maneno
yake ya kejeli. September 25 Mourinho amenukuliwa na vyombo vya habari akitoa kauli bila kutaja jina lakini waandishi wanajua alimlenga kocha wa Arsenal Arsene Wenger.
Kauli ya Mourinho inakuja ikiwa ni siku kadhaa zimepita toka klabu ya Chelsea iifunge klabu ya Arsenal kwa goli 2-0 Mourinho bado anaendeleza kauli zake ambazo ni kama ishara ya kumkejeli Wenger licha ya kuwa hakumtaja moja kwa moja ila kauli hii inatafsiriwa kumlenga Wenger.
“Kila
kocha wa Ligi Kuu Uingereza ana presha na
Ligi, Steve McClaren, Pellegrini na Brendan Rodgers wote wana presha na
mechi za Ligi na tunalazimika kuyafikia malengo, kiukweli nawaonea
huruma kwa sababu ni kazi ngumu. lakini kuna mmoja ambaye hayupo katika
hiyo list lakini yeye anajisikia vizuri na wala hana presha”>>> Mourinho
Kauli ya Mourinho inatafsiriwa imemlenga kocha wa Arsenal Arsene Wenger moja kwa moja kwani ndio kocha ambaye kikosi chake hakifanyi vizuri kwa miaka ya hivi karibuni, hivyo Mourinho anamkejeli Wenger
kwa kumtaja kuwa anaweza akafungwa, akalia lakini akaendelea na kazi
yake kama kawaida tofauti na makocha wengine ambao kama watafanya vibaya
wanaweza fukuzwa kazi.
No comments:
Post a Comment