Bado mechi za Ligi Kuu Uingereza zinaendelea weekend hii, Jumamosi ya September 26 zilichezwa mechi kadhaa ila moja kati ya hiyo ni mechi kati ya Newcastle United dhidi ya Chelsea mechi ambayo ilichezwa katika uwanja wa St James’ Park, uwanja ambao una uwezo wa kuchukua zaidi ya mashabiki 50000.
Klabu ya soka ya Chelsea ambayo ni Bingwa mtetezi wa Ligi hiyo imeendeleza rekodi ya kutopata matokeo mazuri katika Ligi Kuu Uingereza msimu huu. Chelsea kabla ya mechi hii ilikuwa imecheza mechi 6, imeshinda 2, sare moja na kupoteza mechi 3, September 26 imenusurika kufungwa na Newcastle United katika uwanja wa ugenini.
Chelsea ambayo ipo chini ya kocha Jose Mourinho
ilikubali kuruhusu goli mbili katika mchezo huo kabla ya dakika za lala
salama kushituka na kuanza kusawazisha goli hizo, Mechi imemalizika kwa
sare ya goli 2-2. Magoli ya Newcastle United yalifungwa na Ayoze dakika ya 42 na Georginio Wijnaldum dakika ya 60, wakati magoli ya Chelsea yalifungwa na Ramires dakika ya 79 na William dakika ya 87.
Hii ni video ya magoli
No comments:
Post a Comment