Kila nchi ina sheria zake, Sheria za Tanzania sio lazima ziwe Sheria kwenye nchi nyingine, ukweli huo ni sawa hata kwa baadhi ya vitendo… kwa mfano kutukana polisi Tanzania ni kosa kubwa kisheria na pengine ukithubutu kufanya hivyo utakumbwa na matatizo makubwa. Lakini hii kwa wenzetu wa Marekani imekaaje?
Thomas Smith alikamatwa na polisi mwaka 2012 kwa kosa la kuwatukana polisi wa Village of Arena kupitia page yao ya Facebook kitendo ambacho polisi hao walidai kuwa ni kosa kubwa kisheria na hakupaswa kufanya hivyo, na kwa mujibu wa mtandao wa Motherboard Thomas alipost comment kwenye page hiyo ya Facebook iliyosema…
>>> “F* ths f* cops, f* racist basturds an f* all of y’all who is racist”<<< kwenye ukurasa huo wa Facebook akiwa anajibu post iliyopandishwa kwenye page hiyo ambayo aliona imekaa kibaguzi.
Mwanasheria wa Thomas alipinga madai hayo ya polisi kwa kusema kuwa hata Katiba ya Marekani inamruhusu kila mtu kwa uhuru na kwa hisia kukosoa serikali na watumishi wake, na alichokifanya Thomas sio uvunjaji wa Sheria bali ni haki alionayo kikatiba!
Lakini Mahakama inachukuliaje kitendo
cha kutukana polisi hata kama ni kuptia internet kwa kutumia mitandao ya
kijamii? Siku ya ijumaa wiki hii Mahakama ilitoa uamuzi uliosema…
>>>
“Nchi na Mahakama zimekuwa zikihifadhi haki za uhuru wa kujieleza kwa
kila mtu na raia wa nchi hii, na haki hiyo haijahifadhiwa tu kwa kauli
ama hotuba za heshima peke yake. Kwenye nchi hii tuna haki ya kuikosoa
serikali na watumishi wake kwa hisia. Utumiaji wa baadhi ya maneno
haiondoi haki hiyo wala kugeuza kitendo hicho kuwa kinyume na sheria.
Tunatumaini kuwa Arena Police Department na department nyingine za
Polisi kwenye majimbo tofauti wataelewa suala hili.”<<< nukuu kutoka kwenye blog ya Aquino Law Firm iliyokuwa inasimamia kesi ya Thomas Smith.
Thomas Smith sasa yupo huru kuendelea na maisha yake akiwa hana kosa lolote huku kituo hicho cha polisi kimeambiwa kimlipe kijana huyo fidia ya dola 35,000 kwa kumpotezea muda ambayo kwa pesa ya Tanzania tunazungumia fidia ya Tzs milioni 80,500,000!
No comments:
Post a Comment