Staa wa Soka Neymar da Silva Santos Júnior ni mkali ambaye anakamilisha kikosi cha watatu wakali wa Barcelona, yani hapo yuko yeye Luis Suárez na Lionel Messi.
Kwenye Timu inaweza ikatokea Mchezaji
mmoja anapewa nafasi zaidi ya kupiga mashuti ya penati kama ikitokea, au
nafasi ya kupiga faulo.. kuna vitu vinaendelea Uwanjani ambavyo watu wa
nje huenda hawajui…
‘Nimekuwa
napiga sana free-kicks nikiwa na Klabu yangu ya Barcelona na hata
kwenye Timu ya Taifa… Huwa napenda nione nafanya vizuri zaidi kila
wakati, na kila ikitokea nafasi ya kupiga najiweka tayari kushinda goli‘– Neymar.
Majina ya wakali watatu wa Barcelona yanatambuliks lakini Neymar anasema sio kila mtu anaoewa nafasi ya kupiga free-kicks ikitokea >>>> ‘Sina
hofu yoyote kuhusu Messi kupiga free-kicks nyingi zaidi, sisi wote
tunajua yeye ni mkali zaidi na mara nyingi anatupa ushindi wa Barcelona…
ikitokea akinipa nafasi ya kupiga free-kicks nakuwa tayari wakati
wowote, mara nyingi huwa tunajadiliana nani apige lakini mara nyingi
Messi anatusaidia‘ >>> Neymar.
Ninacho kipande cha video, unaweza kucheki free-kicks za Neymar kwenye ubora wake kuanzia mwaka 2011 mpaka 2015.
No comments:
Post a Comment