Kumekuwa na maneno mengi kuhusu kurudi kwa msanii wa Pop wa Uingereza, Adele
kwenye game ya muziki… kama unakumbuka wiki chache zilizopita nilikupa
taarifa kuwa msanii huyo amesogeza mbele tarehe ya uzinduzi wa Album
yake mpya mpaka November mwaka huu lakini tarehe bado haikuwekwa wazi.
Update ilionifikia leo mtu wangu ni kwamba tarehe ya ujio wa album hiyo imeshatangazwa na kwa mujibu wa mtandao wa HITS Daily Double, album mpya ya Adele inategemea kuwa sokoni tarehe 20 November mwaka huu!
Kama wewe ni shabiki mkubwa wa Adele mtu wangu basi update ya taarifa hii ikufikie kokote uliko kuwa Adele anategemea kuachia single yake ya kwanza kutoka kwenye Album yake mpya iitwayo 25 wiki ya kwanza ama wiki ya pili ya November mwaka huu lakini uzinduzi rasmi wa Album yake itakuwa tarehe 20 November 2015… Hii ni good news kwani imepita miaka 4 toka msanii huyo mwenye Grammy 6 aachie album yoyote!
Licha ya hayo tunaambiwa kuwa ’25‘ itakuwa Album inayokamilisha mkataba wake wa sasa na Sony/XL Recording ya Uingereza ila kwa sasa wapo kwenye mipango ya kusign mkataba mwingine na Adele wenye thamani ya zaidi ya Bilion 150 za Kitanzania kwa sasa!
No comments:
Post a Comment